June 10, 2016

Niliachana na Naj kitambo hivyo sina tatizo kabisa na Barakah Da Prince – Mr Blue

Mr Blue amekanusha tetesi zilizowahi kuwepo kwamba ana tofauti na Barakah Da Prince kwasababu muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ sasa ana uhusiano... thumbnail 1 summary
Mr Blue amekanusha tetesi zilizowahi kuwepo kwamba ana tofauti na Barakah Da Prince kwasababu muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ sasa ana uhusiano na Naj aliyewahi kuwa mpenzi wa Kabasyer.


Tetesi hizo zilianza kuvuma baada ya Blue kutoonekana kwenye cover ya wimbo uliowahusisha yeye na Barakah pamoja na Ben Pol ‘Muambie.’


“Yule msichana [Naj] niliachana naye muda mrefu na sina time naye tena na Barakah Da Prince bado ni mdogo wangu tunaheshimiana na tunaongea kila wakati, tuna ukaribu mzuri tu kabisa,” Blue alikiambia kipindi cha Hot Stage cha Jembe FM.

“Lakini wakati wanapiga ile picha mimi kidogo nilikuwa mbali kwenye show nilishindwa kuwepo na ilitakiwa ile picha ipigwe mara moja kwaajili ya tangazo, kwahiyo ndio maana ukaona mimi nimekosa pale,” aliongeza.

“Mimi tayari nimeona nina mke wangu nina watoto na nipo kwenye maisha mengine kabisa na wale wapo kwenye maisha mengine kabisa.”

Msikilize hapo chini.i.


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments