May 03, 2016

NO WAY OUT 2,ALBUM YA MWISHO KWA RAPA PUFF DADDY.ANATAKA KUBOBEA KWENYE FILAMU ZAIDI.

Rapa aliyetamba kwenye sanaa ya muziki,huku akijipa majina mengi ya utani “Puff Daddy”-anajiandaa kuachana na muziki na kujikita kwen... thumbnail 1 summary


Rapa aliyetamba kwenye sanaa ya muziki,huku akijipa majina mengi ya utani “Puff Daddy”-anajiandaa kuachana na muziki na kujikita kwenye filamu.

Puff Daddy au Sean Combs kwa sasa anaandaa albamu yake ya mwisho inayokwenda kwa jina la No way out 2.

“Hii ndiyo albamu yangu ya mwisho,nawekeza nguvu nyingi kwenye albamu hii”,alisema Diddy.

“Ni album nzuri,huwezi kuikosa,Nataka kuona albamu hii inakuwa ua ushindi,nitafanya ziara ya kuitangaza.”

“Nitaondoka,lakini nafahamu nyimbo zangu zitakuwa hewani.Najua jinsi ya kutengeneza muziki utakaoendelea kupendwa kwa muda mrefu.

Michael Jackson, Tupac ,Biggie hawapo lakini nyimbo zao zinaendelea kuishi.”

Combs alitoa album ya kwanza ‘No way out’ mwaka 1997.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments