May 30, 2016

Madawa yakulevya yamenirudisha nyuma, hilo liko wazi – Ibra Da Hustler

Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, amewataka wasanii wenzake kukaa mbali na matumizi ya Madawa ya kulevya. Rappa huyo ambay... thumbnail 1 summary
Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, amewataka wasanii wenzake kukaa mbali na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Rappa huyo ambaye alikaa rehab kwa muda mrefu ili kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, ameiambia Bongo5 kuwa matumizi ya Madawa ya kulevya yamesabisha apoteze dira ya maisha yake.

“Kusema kweli Madawa ya kulevya yamenirudisha nyuma sana, sitaki kuzungumza mengi nadhani hilo liko wazi,” alisema Ibra.

“Mimi sikuwa hivi, niweyumba sana, ndio maana napenda kusema kila kitu kwenye maisha kinatokea kwa sababu, na wenzangu wajifunze kupitia mimi, na kwa wale wenzangu ambao walikubwa na matatizo kama yangu,” aliongeza.

Ibra amesema kwa sasa ameacha kabisa matumizi ya Madawa ya kulevya huku akidai sasa hivi anatumia pombe na sigara tu.

cr: bongo5

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments