May 17, 2016

FA ya Uingereza imezipiga faini Chelsea na Tottenham Hotspurs

Chama cha soka nchini Uingereza FA May 16 kimetangaza adhabu kwa vilabu vyaChelsea na Tottenham amabavyo vinatoka jiji moja la London, FA wa... thumbnail 1 summary

Chama cha soka nchini Uingereza FA May 16 kimetangaza adhabu kwa vilabu vyaChelsea na Tottenham amabavyo vinatoka jiji moja la London, FA wametangaza uamuzi wa kuvipiga faini vilabu hivyo kutokana na kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

FA imetangaza kuipiga faini Chelsea ya pound 375,000 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 ya kitanzania, wakati klabu ya Tottenham Hotspurs imepigwa faini ya pound 225,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 700 za kitanzania, maamuzi yamefanyika kutokana na wachezaji wa timu hizo kufanyiana vitendo visivyo vya kinidhamu wakati wa mchezo dhidi yao.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa Stamford Bridge ilimalizika kwa sare ya goli 2-2, lakini muamuzi alitoa jumla ya kadi za njano 12, hata hivyo mapema mwezi huu Dembele waTottenham alifungiwa mechi sita kutokana na kumpelekea vidole Diego Costa waChelsea machoni kwa makusudi.

TUKIO LA DEMBELE ALILOMFANYIA DIEGO COSTA WAKATI WA MCHEZO HUO

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments