April 19, 2016

Fabregas kaweka wazi kosa lililomuondoa Jose Mourinho Chelsea, lakini bado wanawasiliana

Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas amefunguka na kueleza lililomfanya kocha wa zama... thumbnail 1 summary
Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas amefunguka na kueleza lililomfanya kocha wa zamani wa klabu ya hiyo Jose Mourinho atimuliwa kazi mwezi December, licha ya kuipatia Ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.

Fabregas ameweka wazi wakati akifanya mahojiano na kituo cha tv cha Sky Sportskuwa, bado anawasiliana na kocha wake wa zamani wa Chelsea na siku zote huwa anawalaumu wachezaji wa Chelsea kwa kumuangusha na kusababisha apoteze ajira yake Stamford Bridge.

Fabregas na Jose Mourinho

“Na muheshimu sana Mourinho na bado huwa tunawasiliana, kosa lake kubwa alilolifanya Chelsea ni kutuamini kupita kiasi na kutupa mapumziko ya mara kwa mara, kwa sababu tulikuwa mabingwa, hiyo ndio sababu iliyomfanya aondoke” >>>Cesc Fabregas

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments