March 31, 2016

Zitto Kabwe: Tanzania Kunyimwa Fedha ni Matokeo ya Ubabe wa CCM

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema MCC kuinyima fedha Tanzania ni kwa sababu ya ubabe wa CCM na kwamba, sasa watu wasivikwe kot... thumbnail 1 summary
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema MCC kuinyima fedha Tanzania ni kwa sababu ya ubabe wa CCM na kwamba, sasa watu wasivikwe koti la uzalendo kwa jambo hilo.




Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Zitto aliandika kuwa: “Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi waliochagua viongozi wao Oktoba 25, 2015. 




“Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM, kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar.




“Haina mahusiano yeyote na uhuru wa nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. Nawasihi Watanzania kuelewa kwamba CCM ndio imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila kuufanya ni mzigo wa nchi.”




Aliandika pia kwamba: “Zanzibar inatazamwa kama Zanzibar, kwa wenye maono mafupi. Nilipata kuwaambia viongozi wenzangu kwamba tishio kubwa zaidi la kutoshughulikia mtanziko wa Zanzibar ni upotoshaji. 




“Tutajikuta tunaacha kushughulika na masuala ya maendeleo kwa kipindi kirefu kidogo. Tabia ya kitanzania ya kupenda ‘shortcuts’ (njia za mkato) itatugharimu sana. You can’t just ignore Zanzibar and move on. You just can’t (huwezi ukaipuuzia Zanzibar na ukaendelea tu, huwezi).” 




Pia Mbunge huyo aliandika kuwa: “Serikali ya Marekani imesitisha mahusiano na Serikali ya Tanzania kwenye miradi ya MCC. 


“Hivyo Tanzania itakosa Sh. trilioni moja ambazo zilikuwa zimeelekezwa kwenye umeme na umeme vijijini. 


“Sababu? Zanzibar na Cybercrime Act. Siku si nyingi tutawasikia Umoja wa Ulaya nao. Nasubiri kusikia Serikali ya Rais Magufuli itasema nini. 




“Suala la Zanzibar likitazamwa kibabe kwa kuwa watawala wana maguvu nchi itaingia kwenye matatizo makubwa sana ya ndani bila kujali misaada inakatwa au la. Sipendi misaada. Sipendi mataifa ya kigeni kuingilia masuala yetu ya ndani. 




“Lakini Tanzania sio kisiwa, tunaishi ndani ya jamii ya kimataifa. Kuna mambo lazima tufanye kwa kuzingatia misingi ya kidunia. Zanzibar ni moja ya jambo hilo. Tusiweke kichwa kwenye mchanga kama mbuni.”




Naye Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje wa Chama Cha ACT-Wazalendp, Theopister Kumwenda, alisema uamuzi huo wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini. 




Alisema ACT-Wazlendo inatambua kuwa katika kipindi hiki Tanzania inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwamo MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. 





Alisema MCC imekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijijini

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments