February 24, 2016

Kama ni mtumiaji wa Instagram Tanzania inabidi uyajue haya mabadiliko.

Walisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa kijamii wa Instagram na ndio maana naamini mabadiliko yaliyo... thumbnail 1 summary
Walisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa kijamii wa Instagram na ndio maana naamini mabadiliko yaliyotokea yanatakiwa kuwafikia Watanzania.

Kama hujagundua kwenye page yako ya Instagram ni kwamba kila unapopost video ya sekunde 15 kama ulivyo utaratibu wa kawaida wa Insta, mabadiliko mapya yaliyofanywa na mamlaka ya mtandao huu wa kijamii ni kukupa fursa wewe na followers wako kuonavideo uliyopost imetazamwa na watu wangapi kama inavyoonekana hapa chini.


Kwenye mabadiliko haya ya Instagram, mtandao wa kijamii wenye watumiaji zaidi ya milioni 400, likes hazitoonekana mpaka ubonyeze sehemu yenye idadi ya views ndio itakupeleka kuona likes za hiyo post.


Mpango huu mpya wa Instagram ulitangazwa zaidi ya siku kumi zilizopita na mabadiliko nimeanza kuyaona Tanzania kuanzia February 22 2016.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: