February 27, 2016

Baada ya Blatter kutawala kwa miaka 18 FIFA yapata Rais mpya leo

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo Ijumaa ya February 26 ndio siku lilifanya uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais wa kuziba pengo la Se... thumbnail 1 summary

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo Ijumaa ya February 26 ndio siku lilifanya uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais wa kuziba pengo la Sepp Blatter aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo kwa miaka 18. FIFA imefanya uchaguzi na aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) kwa miaka saba Gianni Infantino kushinda nafasi hiyo.

Gianni Infantino ameshinda raundi ya pili ya nafasi hiyo ya Urais kwa jumla ya kura 115, na kumzidi mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kwa zaidi ya kura 27, wakati Prince Ali bin al-Hussein akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na kura nne. Infantino ambae ni mwanasheria kitaaluma anatokea Valais maili chache kutoka makazi ya Sepp Blatter yalipo.

Infantinho anakuwa Rais wa FIFA wa tisa, baada ya Sepp Blatter kutawala wadhifa huo kwa mihula mitano kabla ya kujiuzulu mwishoni mwa mwaka jana na kufungiwa miaka sita kutojihusisha na soka. Infantinho pia anauwezo wa kuongea lugha za kiingereza, kiitaliano na kifaransa.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: