January 10, 2016

Vitu vitano vinavyoweza kukushangaza Zanzibar, kuna hoteli huwezi kulala hata uwe tajiri vipi …

Mtu wangu wa nguvu wakati Kombe la Mapinduzi likiwa limesimama kwa mapumziko ya siku moja kabla ya Jumapili ya January 10 kuendelea kat... thumbnail 1 summary

Mtu wangu wa nguvu wakati Kombe la Mapinduzi likiwa limesimama kwa mapumziko ya siku moja kabla ya Jumapili ya January 10 kuendelea katika hatua ya nusu fainali. Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kutembelea maeneo tofauti tofauti hapa visiwaniZanzibar, lengo likiwa ni kukujuza baadhi ya vitu ambavyo huenda ukawa huvijui kuhusuZanzibar. Haya ni mambo matano ambayo yanaweza yakakushangaza kama umefikaZanzibar kwa mara ya kwanza na umezoea kuishi maeneo kadhaa ya mikoa ya Tanzaniabara basi huenda hii ikakushangaza.

1- Kama umezoea kwenda maeneo ya Kariakoo kununua bidhaa na kuwekewa katika mifuko ya plastic, basi hilo Zanzibar hakuna mifuko laini ya plastic inayoruhusiwa. Ukinunua bidhaa kuna aina ya mifuko ambayo utapewa kama mifuko ile ya karatasi ya kaki, lakini usitegemee kuona mifuko laini ya plastic ikizagaa au kutumika.


2- Daladala au mabasi ya abiria kwa Zanzibar hayaruhusiwi kusimamisha abiria, hivyo mara nyingi husimamisha abiria pale mahali ambapo hakuna askari. Ikitokea wamesimamisha abiria halafu wanakaribia eneo kuna trafiki basi konda atakuomba ukae vizuri tu ili gari isionekane kama imejaa kukwepa kusimamishwa na askari.


3- Vesper ndio pikipiki zinazotumika kwa wingi Zanzibar ila sio kubeba abiria ni kwa safari binafsi, usishangae kuona siku ikipita bila kuona aina nyingine ya pikipiki kamaBoxer, Sanlg na nyinginezo na ukiziona basi ni kwa safari binafsi na sio kama Boda Boda.


4- Kama ulikuwa unajua Hiace na Coaster ndio gari pekee zinazoweza kutumika kubeba abiria kama daladala basi utakuwa umekosea, Zanzibar hata Canter zimeruhusiwa kubeba abiria ila kwa mfumo ambao wamezitengeneza na kuziwekea mabenchi ndani na kazi ya kubeba abiria inaendelea kama kawaida.



5- Hili ndio kubwa lililonishangaza mtu wangu, baada ya kufika hoteli inayoitwa Amani Kendwa ambayo ipo pembezoni mwa fukwe za bahari ya Indi hapa Zanzibar nje kidogo ya mji wa Unguja. Hii ni hoteli ambayo maalum kwa waitaliano tu kwa mtu mwingine huruhusiwi kulala ila unaweza ukaenda kupata lunch au dinner hiyo haina neno. Utaratibu wa muitaliano kupata nafasi ya kulala hapo ni ana book moja kwa moja akiwa Italia na kupelekwa hapo, hivyo watu wa mataifa mengine hawapokelewi kwa kulala zaidi ya kupata chakula. Hata kama ni muitaliano ila umekuja kuomba ukiwa Zanzibar huwezi ruhusiwa kulala.

Sehemu ya muonekano wa fukwe za Amani Kendwa nyakati za usiku

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: