August 19, 2015

Mpenzi Wangu Simuelewi, na Nimekuta Picha yake FB imewekwa na Msichana

Nina mpenzi wangu tunakaribia kumaliza mwaka sasa. Kukutana kwetu ni mara chache sana kutokana na masomo. Kusema kweli tokea tumeanza... thumbnail 1 summary
Nina mpenzi wangu tunakaribia kumaliza mwaka sasa. Kukutana kwetu ni mara chache sana kutokana na masomo.

Kusema kweli tokea tumeanza mahusiano sijawahi pokea hata shs 10 toka kwake. Hapo mwanzo tulikuwa tunawasiliana vizuri kipindi nikiwa chuo kutokana na pesa ninayotumiwa na mama yangu nikifunga chuo mawasiliano yanapungua sababu kutokuwa na pesa ya kununua vocha.

Nikimuelezea hiyo hali anasema haiwezekani Sasa kabadilika, nikimuuliza anasema yupo kawaida.

Kinachonitatiza ni kwamba juzi kati nilikuta picha yake FB imepostiwa na mdada fulani, comments zinaonyesha huyo dada na aliyeko kwenye picha ambaye ni mpenzi wangu ni wapenzi.

Kumuuliza mpenzi wangu anadai hajui ni kwanni huyo dada kapost hiyo picha na kwamba sio wapenzi ila wanafahamiana.

Jamani nisaidieni maana roho inauma sana

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: