July 26, 2015

UTATA MPYA MTOTO WA DIAMOND,KIZAA ZAA YAANI NI SHIIDA

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa katika pozi na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. thumbnail 1 summary
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa katika pozi na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Utata mpya umeibuka wakati mama kijacho wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, akitarajiwa kujifungua muda wowote kutoka sasa, ishu ni juu ya uraia wa mtoto atakayezaliwa.


TUJIUNGE NA MTU WA NDANI


Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia hiyo zilidai kwamba, utata umezidi kuigubika familia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ndugu wa pande zote kuendelea kuvutana juu ya Zari ajifungulie nchi gani kati ya Tanzania, Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’.




Utata huo umevuja wakati paparazi wetu akiwa katika mishemishe za kutaka kujua Zari alipo kwa sasa na atajifungulia katika hospitali ipi ndipo alipopenyezewa ‘ubuyu’ kwamba hadi sasa kuna utata mkubwa katika familia hiyo.


MABISHANO YA URAIA


Chanzo kilimweleza mwanahabari wetu kuwa, kikubwa ni mabishano ya uraia na sehemu sahihi ya kujifungulia mtoto huyo.


Kilidai kwamba, suala hilo limekuja kufuatia ndugu wa Zari kutaka ajifungulie Sauz jambo ambalo Diamond na familia yake wamekuwa wakilipinga vikali.




ZARI NJIA PANDA


Ilisemekana kwamba, kwa upande wake Zari amekuwa njia panda kutokana na shinikizo hilo huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye akisisitiza kuwa lazima Zari ajifungulie Bongo ili amuhudumie mkwe wake huyo.


“Yaani ndugu wa Zari wanampa Diamond wakati mgumu sana kutokana na kuendelea kung’ang’ania Zari akajifungulie kwao (Sauz ambako kuna ndugu wengi) wakati furaha ya Diamond ni kuona mtoto akizaliwa Bongo.


DIAMOND ACHACHAMAA


“Unaambiwa Diamond amechachamaa vibaya, alipoona hawezi kutumia nguvu ikabidi atumie ushawishi kwa ndugu wa Zari ili wakubali ajifungulie Bongo lakini wale ndugu wanasema wako tayari kumtumia hata ndege kwa sababu yupo Bongo, arudi Sauz ambako kuna daktari wao wa familia.


HUYU HAPA DIAMOND


Paparazi wetu baada ya kunyaka utata huo alimtafuta laivu Diamond kwa kujiridhisha zaidi juu ya hilo ambapo baada ya kumpata alifunguka kwamba, kipindi hiki kuna mambo kibao yanaibuka kila kukicha jambo linalomshangaza.




Alisema kuwa utata huo alishamalizana nao ndiyo maana hadi muda huu Zari yupo Dar kwa ajili ya kujifungua.


“Ninachoweza kusema kwenye maisha ya kawaida huwezi kuwazuia watu kuongea jambo wanaloliwaza wao.


“Hayo mambo ya utata nimeshayamaliza ndiyo maana kwa sasa Zari yupo White House (nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Madale jijini Dar) akisubiria saa ya kujifungua.




“Kwangu namuomba Mungu ajifungue salama maana mtoto ni miongoni mwa vitu nilivyotamani kitambo,” alisema Diamond huku akiwashukuru Watanzania wote wanaoendelea kumuunga mkono kwenye muziki wake.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: