May 15, 2015

Mapinduzi ya Burundi: Rais Pierre Nkurunziza Ahojiwa na Kituo cha habari cha Burundi RTBN.......Asema Yupo Tayari Kumsamehe Mwanajeshi Atakayesalimu Amri

Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita. thumbnail 1 summary
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.

Katika mahojiano hayo ambayo Shirika la habari la Reuters lilifanikiwa kuyanukuu, Rais Nkurunziza amesema yupo tayari kumsamehe mwanajeshi yeyote atakayekubali kusalimu amri.

''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi, nawashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.Alinukuliwa akisema.

Muda mfupi baada ya mahojiano hayo, vita kali ya majibizano ya risasi iliibuka karibu na kituo hicho cha habari baina ya wanajeshi watiifu kwa rais huyo na wale waliotangaza kumpindua.

Hali hiyo ilikilazimu kituo hicho kuzimwa na kisha kufunguliwa tena baada ya mapigano kuisha

Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba wanajipanga kukiteka kituo hicho cha habari cha RTNB kilicho chini ya udhibiti wa wanajeshi watiifu kwa Rais

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: