February 07, 2015

BOBBY BROWN: SIWEZI KUONDOA MASHINE YA KUPUMUA, MUNGU ATAMWOKOA MWANANGU BOBBI


Bobby Brown akipozi na binti yake Bobbi Kristina.

Marehemu Whitney Houston akiwa katika pozi na mwanaye Bobbi Kristina mwaka 2007.

Bobbi Kristina katika picha ya pamoja na patna wake Nick Gordon.
HALI ya binti wa Whitney Houston, Bobbi Kristina imeendelea kuwa mbaya mpaka madaktari kumshauri baba yake Bobby Brown wamuondolee mashine inayomsaidia kupumua.
Bobby Brown amekataa katakata mashine hiyo kuondolewa maana anaamini katika miujiza ya Mungu kumponyesha mawanaye huyo mwenye miaka 21.
Hisia za Bobby zimetofautiana na madaktari walioshauri mashine hizo ziondolewe maana Bobbi hapati nafuu tangu alipohamishiwa kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory majuzi Jumanne.
Bobbi Kristina alikutwa akiwa amepoteza fahamu Jumamosi iliyopita ya Januari 31, mwaka huu baada ya kukutwa kwenye jacuzzi akiwa hajitambui na mpaka sasa bado hajapata fahamu.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: