January 04, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA


Bwana George Mcheche Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteuaBwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: