October 24, 2014

MGOMBEA 2015 ANASWA NA DENTI GESTI

HILI nalo janga!  Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jij... thumbnail 1 summary
HILI nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la  mzee Beno amenaswa
akiwa chumba cha gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar, Ijumaa ‘kubwa’ lina mkanda wote.
Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mzee Beno akificha sura kwa aibu ili asipigwe picha baada ya kufumaniwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.
WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema  alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo.
Akidhibitiwa baad ya kufumaniwa.
USHUSHUSHU
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno  (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.
MBALI NA UJUMBE
Ikadaiwa kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye mazuri siku za usoni.
Mfanyabiashara na denti huyo wakijutia kwa kitendo walichokifanya.
BINTI ATII AMRI YA WAZAZI
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.
NI KAMA WALISEMA
“Mtu gani mama?”
Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”
Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”
Mama: “Anaitwa nani?”
Mfanyabiashara huyo akisihi kuachiwa baada ya kufumaniwa.
Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli?  (kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku moja.”
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”
MTEGO
Ikadaiwa kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda wakutane huko gesti ili  wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo, mzee akashindwa kujiongeza.
Binti akiwa na mzazi wake na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo alishafika zamani gani na kumsubiri.
Bw. Beno akiwa nje ya gesti hiyo iliyopo kimara suka mara baada ya kufumaniwa.
Baada ya muda, binti alituma meseji kwa mama yake akisema mambo tayari, wapo ‘weupe pee’ (hawana nguo). Ndipo mama huyo akachukua timu yake na kuvamia gesti hiyo kwa ajili ya kulianzisha.
OFM YAKATIZA MITAANI, YAKUMBANA NA KASHESHE
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ilikuwa ikikatiza mitaani kusaka matukio kwani ni ada yake, ndipo walipoibukia eneo lenye gesti hiyo na kukumbana na kasheshe hilo la nguvu.
 “Hawa wazee ndiyo wale ambao wanaharibu watoto wa watu huku yeye wanawe wakisoma vizuri na hakuna anaowaharibia masomo yao,” alisikika akichonga mama huyo.
Akaendelea: “Jamani nawaomba njooni na makamera yenu yote hapa.”
OFM YAPATA NGUVU
Kufuatia maneno ya mama, OFM walipata nguvu na kuanza kupiga picha za kumwaga kwa ajili ya kumbukumbu.
Huu ni usafiri aliokuja nao mzee Beno kwenye gesti hiyo.
MGOMBEA ASEMA NENO
Huku akiwa amekaa kwa tafakuri ya kina, mzee Beno alisema ameumbuka na kuitaka familia ya mwanafunzi huyo kumalizana kifamilia nje ya gesti hiyo huku akiwaomba OFM chondechonde wasiitoe habari gazetini.
Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitamboni, mwanamke huyo alisema hawajamalizana chochote hivyo OFM inaendelea kufuatilia sakata hilo.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: