August 04, 2014

TETESI ZA USAJILI ULAYA: BRENDAN RODGERS AKANUSHA KUMSAJILI MTUKUTU MARIO BALOTELLI

+6 Tabasamu bab kubwa: Mario Balotelli (kushoto, akiwa na Mamadou Sakho) hawataungana Liverpool mwezi huu. KOCHA wa Liverpool... thumbnail 1 summary
All smiles: Mario Balotelli (left, with Mamadou Sakho) won't be moving to Liverpool this month
Tabasamu bab kubwa: Mario Balotelli (kushoto, akiwa na Mamadou Sakho) hawataungana Liverpool mwezi huu.KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amekanusha
tetesi za kutaka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan, 'Mtukutu' Mario Balotelli.
Rodgers alihusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City baada ya kumzungumzia Balotelli wakati maandalizi ya mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya AC Milan.
Liverpool wapo sokoni kutafuta mshambuliaji baada ya dili la kumsajili Loic Remy kushindikana, lakini Rodgers amekanusha kuitaka saini ya Balotelli.
Rubbish! Reds manager Brendan Rodgers said Balotelli 'categorically' won't be joining the Anfield club
Uvumi!  Brendan Rodgers alisema Balotelli hatajiunga Anfield
Let go, please! Jordan Ibe grabs hold of Balotelli's shorts during Liverpool's 2-0 win against AC Milan

Tuli tuli! Jordan Ibe akivuta bukuta ya  Balotelli katika ushindi wa Liverpool wa mabao 2-0 dhidi ya AC Milan.
Gone: Luis Suarez left the club earlier this summer in search of trophies in Spain with Barcelona 
Amesepa: Luis Suarez aliondoka klabuni mapema majira ya kiangazi akienda kutafuta makombe Hispania.

Wakati anazungumzia mechi ya fainali ya kombe la kimataifa dhidi ya Manchester United leo jumatatu, Rodgers alisema: "Kiukweli nawaambieni kwamba hatajiunga Anfield.
'Niliulizwa swali kuhusu Balotelli na nilizungumzia jinsi alivyo na kipaji na jinsi alivyo mchezaji mzuri.
'Ni mchezaji wa ajabu, lakini ni mchezaji wa AC Milan, nilitoa tu maoni yangu, lakini haimaanishi nitamsajili.'
Rodgers alisema Man United inaweza kuibuka tena katika ligi kuu England msimu ujao chini ya kocha mpya Louis Van Gaal baada ya kumaliza nafasi ya 7  wakati wa kocha David Moyes.
Alitabiri mechi ya ushindani baina ya timu mbili hasimu itakayopigwa leo mjini Miami, lakini alisisitiza kuwa haitakuwa na maana kubwa na kutabiri mbio za ubingwa England.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: