August 24, 2014

Mtuhumiwa kesi ya Swissport alalamikia unyama wa polisi …Adai kuingizwa Chupa sehemu za haja kubwa

ya wizi wa simu inayowakabili wafanyakazi sita wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua mizigo ya Swissport, imechukua sura mpya baada ya ms... thumbnail 1 summary
ya wizi wa simu inayowakabili
wafanyakazi sita wa Kampuni ya Kupakia
na Kupakua mizigo ya Swissport,
imechukua sura mpya baada ya
mshitakiwa Hashim Idd (49) kudai
amefanyiwa vitendo vya unyama
alipokuwa anachukuliwa maelezo na
Polisi.

Hata hivyo, Mahakama ya Wilaya ya Ilala
imepokea kama kielelezo maelezo ya onyo
ya mshtakiwa huyo baada ya kukataa
maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo
kama kielelezo, kwa madai kuwa
alilazimishwa kusaini maelezo ambayo
hakuyatoa polisi wakati akihojiwa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi
Hassan Juma, Idd alidai mbali na
kulazimishwa kusaini maelezo hayo
aliingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa
na askari polisi walikuwepo katika
chumba ambacho alikuwa akichukuliwa
maelezo katika kituo cha polisi cha
Uwanja wa ndege ili aweze kukubali
mashitaka hayo ya wizi.
Hata hivyo, mahakama hiyo iliyakataa
maelezo hayo kwa madai kuwa ni
maelezo ya kutunga na hayana ushahidi.
Katika kesi hiyo, shahidi Phraim alidai
kuwa siku ya tukio, Januari 31 mwaka
huu alipewa taarifa za kesi ya wizi wa
simu kutoka kwa mkuu wa upelelezi wa
kituo hicho. Alidai
wizi huo ulitokea Januari 27 mwaka
huu, saa 7:10 mchana  ambapo boksi moja
lenye simu 460 aina ya Tecno na Itel
liliibwa kutoka katika ndege ya Qatar
Airways iliyokuwa ikitoka nchini China.
Washitakiwa hao ni Hamada Mohammed
(42), Haji Waziri (26), Yusuph Muhangwa
(33), Hashimu Idd (49), Ally Omary (33) na
Hamisi Othuman (29) ambao
walituhumiwa kuiba simu zenye thamani
ya Sh milioni 19.4 mali ya Chemchem.
Washitakiwa wapo nje kwa dhamana.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: