August 31, 2014

Epl: matokeo ya mechi zote na Kilichoikuta Man City mbele ya Stoke City hiki hapa

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City leo wamekula mweleka katika mbio za kupigania ubingwa wao kwenye mechi dhidi... thumbnail 1 summary

IMG_6882.PNG


Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City leo wamekula mweleka katika mbio za kupigania ubingwa wao kwenye mechi dhidi ya Stoke City.

City wakiwa uwanjani kwao Etihad Stadium wamepokea kipigo cha 1-0 kutoka kwa vijana wa kocha wao wa zamani Mark Hughes.

Alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Mame Biram Diouf ndio aliyewamaliza Man City kwa goli zuri dakika kadhaa baada ya kipindi cha pili kuanza.
Diouf alichukua mpira uliokolewa golini kwake na kumpita Fernandinho kisha akakimbia na kumtoka Kampany na kupiga shuti lilompita tobo golikipa Joe Hart.
Matokeo ya mechi nyingine za EPL yapo kama ifuatavyo: Sunderland 0-1 QPR, Palace 3-3 Newcastle, West Ham 1-3 Southampton, Swansea 3-0 West Brom
IMG_6881.JPG

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: