June 15, 2014

WEMA SEPETU ADAKA MIMBA YA DIAMOND PLATNUMZ

'Beautiful Onyinye' na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na... thumbnail 1 summary

'Beautiful Onyinye' na kipenzi cha
Diamond, Wema Sepetu sasa ni mjamzito.
Baada ya misukosuko ya muda mrefu
ikiwemo kuporwa na wasichana
wenzake penzi lake la Diamond, sasa
Wema amepata kile alichokuwa akikililia

kwa muda mrefu....
Chanzo cha habari hii kutoka kwa
marafiki wa Diamond kimedai kuwa
Wema amenasa ujauzito na kugundulika
hivyo walipokuwa Afrika Kusini kwenye
tuzo za MTV-MAMA na kumfanya
Diamond achanganyikiwe kwa furaha....
Kwa mujibu wa chanzo
hicho, inadaiwa
kuwa Diamond kwa sasa kawa kama
mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana
na taarifa hizo njema na tayari
ameshaanza maandalizi ya kijacho
chake....
Kugundulika kwa ujauzito wa Wema ni
baada ya kuanza kujisikia vibaya
walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo
kichefuchefu na kizunguzungu
alipokuwa hotelini alipofikia na
kulazimika kwenda hospitali kwa
uchunguzi zaidi....
Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa
na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini
waliyekuwa naye huko Afrika Kusini
kumpa sapoti Diamond na madaktari
ndiyo waliomjuza
kuwa anakiumbe
tumboni cha wiki 7...
Taarifa za madaktari hao zilimfanya
Wema awe kama mwehu aliyepagawa
na kurudi hotelini kwa mumewe
Diamond huku akiwa na tabasamu
ambalo hapo awali Diamond hakuwahi
kuliona....
Inasemekana kuwa mpaka sasa siyo
Diamond wala Wema aliyewaambia
wazazi wake kuhusiana na mimba hiyo
zaidi ya watu wa karibu wa wawili hao
waliowasindikiza Afrika Kusini.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: