June 11, 2014

Malawi Wameanza Chokochoko Ndege yao Yaonekana Ikifanya Doria Ileje, Wananchi Wataaruki

MBUNGE wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ameomba Serikali ieleze juu ya ndege kutoka Malawi, ambayo imekuwa ikitia hofu wananchi wa Ileje, ... thumbnail 1 summary


MBUNGE wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ameomba Serikali ieleze juu ya
ndege kutoka Malawi, ambayo imekuwa ikitia hofu wananchi wa Ileje, kwa
kuzunguka angani kilamara.Mbunge huyo alisimama kutoa hoja hiyo baada
ya kipindi cha maswali na majibu na kuomba mwongozo wa Spika, Anne

Makinda kuhusu suala hilo. Kibona alisema:"Nazungumzia jambo mahsusi
linalotokea katika mpaka wa Tanzania na Malawi katika Jimbo la Ileje.
Kwa sasa kuna ndege kutoka nchi ya Malawi inazunguka katika vijiji
jirani na tayari imeleta hofu kwa wananchi; na watoto hawawezi kusoma.
Ninaomba mwongozo wako kama nipo sahihi. Naitaka Serikali kwanza
ieleze ile ndege inatoka wapi na inafanya nini; na Pili naitaka
Serikali imfahamishe Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhusu ndege hiyo ili
naye awafahamishe wananchi
ili wasiwe na hofu".Mbunge huyo alisema
aliamua kuleta hoja hiyo bungeni, kwa kuzingatia uhusiano uliopohivi
sasa baina ya Tanzania na Malawi. Baada ya maelezo hayo ya Kibona,
Spika alisema:"Suala la Mheshimiwa Kibona linahitaji kufanyiwa kazi
sana". Serikali inaendelea na vikao vyake na itampatia majibu Kibona

baadaya kutafakari na kujadili suala hilo.
ACHA MAONI YAKO HAPO CHINI

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: