May 19, 2014

Q CHILLAH AELEZEA NINI KILITOKEA JUU YA KIFO CHA ADAM KUAMBIANA

Msanii wa muziki Aboubakar Katwila aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu Adam PhilipKuambiana, amedai kuwa kabla ya kifo cha rafiki ya... thumbnail 1 summary


Msanii wa muziki Aboubakar Katwila aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu Adam PhilipKuambiana, amedai kuwa kabla ya kifo cha rafiki yake, alilalamika
maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo na kuharisha damu. Profesa Jay,JB ,Q Chillah wakiwa na marehemu Adam Philip Kuambiana enzi za uhai wake maeneo ya Coco Beach jijini Dar Akizungumza na Ijumaa Wikienda alisema: “Jana (ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku wa
manane lakini bado akiendelea kulalamika maumivu ya tumbo. Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa anaendelea kunywa pombe wakati anaumwa? Akawaambia wamuache. Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda kulala chumbani kwake huku tukiahaidiana kwamba itapofika saa 3:00 asubuhi tuwe tayari kwa kwenda location. Lakini ilipofika muda huo sisi tukiwa tayari kwa safari tulikwenda kugonga mlango wa chumba chake bila mafanikio.
Chakushangaza alisikika sauti yake kwa mbaili, kwa bahati nzuri mlango wake ulikuwa wazi, mmoja akaingia ndani na kumkuta ameanguka chooni na hajiwezi. Neno lake la mwisho alisema kwamba anajisikia kuishiwa nguvu na anaharisha damu. Kutokana na hali yake hiyo mbaya tulimbeba na kumlaza kitandani kasha tukatafuta gari na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma ambapo daktari alisema alishafariki dunia muda mrefu,”alisema Q Chillah Q Chillah ambaye alikuwa mhusika na filamu mpya ya ‘Joto’ ya marehemu Adam Kuambiana amedai kuwa marehemu alisema kuwa filamu hiyo ambayo waalikuwa wanaifanya ingekuwa ya mwisho kwake. “Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo ilikuwa
apate fedha nyingi sana kwa sababu ni yak wakemwenyewe na ni kali mno, amecheza vizuri akinishirikisha mimi. Lakini ndiyo hivyo tena  imeishia katikati sijui ni nani ataiendeleza maana mwenyewe katuachia majonzi,” aliongeza Q Chillah. Historia fupi ya Adam Kuambiana Marehemu Adam Philip Kuambiana alizaliwa mwaka 1976 Ifunga Mkoani Iringa, alipata elimu ya msingi katika shule ya Mlimani Jijini Dar na
baade sekondari ya Tambaza kisha akahamia jijini Nairobi kwenda kusoma kidato cha tano na
sita baada ya hapo alielekea Afrika Kusini kupata elimu ya filamu na baada hapo alikuwa fiti katika
uwigizaji, uongozaji na pia alikuwa mwandishi wa miswada ya filamu. Miongoni mwa filamu ambazo amerehemu ametia mikono yake kwa kiwango kikubwa ni pamoja na Fake Pastor, Life of Sandra, Faith ,More Fire, Scora, Lost Son, My Fience, Jesica, Basilisa, No Body, Chaguo Langu na nyingine nyingi. 


SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: