May 09, 2014

BIFU LAZIDI KUSHIKA KASI!! HUU NI USHAIDI MWINGINE WA WEMA, KAJALA KUMUIBIA BWANA AKE!!

Stori: IMELDA MTEMA Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili! Hatimaye Wema ... thumbnail 1 summary
Stori: IMELDA MTEMA
Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili! Hatimaye Wema Isaac Sepetu amenasa ushahidi wa
aliyekuwa rafikiye kipenzi, Kajala Masanja wa kumwibia aliyekuwa bwana’ke, Clement au CK, yule kigogo wa ikulu.
Wema Sepetu.
MIL. 13 KISINGIZIO TU
Habari za mjini kwa wiki nzima ni kusambaa kwa ujumbe mfupi (SMS) za kimapenzi za Kajala na CK ambazo sasa zimefunua kisa kamili cha mastaa hao
kuhitilafiana huku Sh. Milioni 13 zikiwa kisingizio tu.
WEMA ALIKUWA ANATAFUTA USHAHIDI?
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na mastaa hao, kupatikana kwa meseji hizo ni kama mpango wa Mungu, kwani sasa kitendawili kimeteguka.
Baadhi ya meseji zilizonaswa.
“Wema alikuwa anatafuta ushahidi kama kweli Kajala anatembea na CK hivyo sasa amepata ushahidi.
“Mwenye macho haambiwi tazama na kama hujui kusoma hata picha huoni? Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako!” Kilisema chanzo hicho.
Habari za ndani zilieleza kuwa meseji hizo zilikutwa kwenye simu ya CK na mwanamke mwingine ambaye naye anadaiwa kutoka na kigogo huyo, aliyetajwa kwa jina moja la Naima aliyekwenda kumbwagia ‘zigo’ Wema kwa ajili ya ushahidi.
Kajala Masanja.
Ilisemekana kwamba Naima alimuomba simu CK kwa kuwa ya kwake ilikuwa mbovu.
Habari zilizidi kudai kuwa baada ya CK kumpa mpenzi wake huyo simu yake, kumbe zile meseji alizokuwa akichati na Kajala alikuwa amesahau kuzifuta ndipo zilipobambwa.
Mpashaji wetu aliweka wazi kwamba meseji zile zilimshangaza Naima kwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawaamini kabisa kama kulikuwa na ukweli wowote kuhusu tuhuma za Kajala kutembea na CK.
NAIMA ACHANGANYIKIWA

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: