April 11, 2014

WASANII WAJANJA NA WENYE MANDELEO HAWATUMII UNGA WANATUMIA MBINU HIZI

Rehema Chalamila ‘Ray C’. INGAWA Rehema Chalamila ‘Ray C’ na Radhid Makwilo ‘Chid Benz’ ndiyo wasanii pekee waliokiri hadharani kuwahi ku... thumbnail 1 summary
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
INGAWA Rehema Chalamila ‘Ray C’ na Radhid Makwilo ‘Chid Benz’ ndiyo wasanii pekee waliokiri hadharani kuwahi kutumia madawa
ya kulevya na kwamba wako katika harakati za kuhakikisha wanaachana nayo, ukweli ulio dhahiri ni kwamba tunao wasanii wengi,
hasa wa Bongo Fleva ambao ni wabwia unga!Wakati vuguvugu la muziki huu linaanza kupamba moto mwanzoni mwa miaka ya 2000, vijana wengi waliibuka, wakifanya kazi nzuri kwa tungo zenye kuelimisha na kwa kiasi kikubwa, walijitahidi kwa vitendo kupinga mtazamo wa watu wengi wazima kwamba aina ile ya muziki ulikuwa ni uhuni.
Kazi kubwa sana imefanyika kuufikisha muziki huu hapo ulipo, kwani wakati wazazi wengi waliwazuia watoto wao kujihusisha na muziki huu kwa madai kuwa ni uhuni, ni kweli kwamba vijana wengi wanamuziki walikuwa na hata sasa wanatumia bangi, tena wakivuta hadharani.
Mkali wa Bongo Fleva nchini, Radhid Makwilo ‘Chid Benz’.
Kwa wazazi, bangi ni kilevi kibaya, chenye kuleta matokeo hasi kikitumiwa, ingawa pia baadhi ya watu wanathibitisha kuwa mmea huo ni dawa. Binafsi ninayo orodha ndefu ya wasanii wanaokula ‘ganja’ na ambao baadhi yao walifanya hivyo mbele yangu, tena bila hofu kwa kuwa muziki wa kizazi kipya ulitufanya kuwa marafiki.
Bangi pia inatumiwa sana na wanasoka, tena hawa ni balaa zaidi. Siyo jambo la ajabu kukuta kikosi cha cha timu yoyote, kikiwa na wavuta bangi kwa asilimia 70-80. Uzoefu wangu unanionyesha kuwa mvutaji wa mmea huu, hasa anayetumia kama burudani, hana madhara kwa watu wanaomzunguka.
Wasanii wana sababu nyingi zinazowafanya wavute, wakidai wanaondoa aibu, wengine wanapandisha mzuka na baadhi yao wakisema inawapa ubunifu mbele ya kadamnasi. Ndiyo maana hata wadada nao hula ‘msuba’.
Ndivyo pia inavyokuwa kwa wanasoka, wapo wanaoamini ukivuta ndiyo unakuwa mzuri zaidi kwa ufanisi uwanjani tofauti na ukiwa hujatumia. Tabia za ukorofi ndani au nje ya uwanja haina uhusiano wowote na bangi.
Wengi wa wale ninaowajua kutumia bangi, bado wapo na  wanafanya vizuri katika game. Lakini kwa namna ya kushtusha kabisa, wasanii wetu wamejikuta katika ulevi mpya, wa kubwia unga.
Huu, tofauti na bangi, hummaliza kabisa mtumiaji, siyo tu kimwili, bali hata kiakili. Ndiyo maana utaona asilimia kubwa ya wanaotumia madawa ya kulevya, afya zao zina mushkeli na hawana mwelekeo wa maisha.
Unga unawafanya wawe wavivu wa kazi, muda mwingi wanapenda wawe ‘wanabembea’. Ninajua, watumiaji hawa wanajiona wao ni wajanja, watoto wa mjini. Katika kufanya kazi hii ya kuandika habari za burudani, niliwajua wasanii wengi wenye uwezo, lakini wanapotea taratibu sababu hivi sasa wanakula unga.
Mtu mjanja hawezi kubwia unga. Mjanja ni yule anayejua kuwa ni kazi pekee ndiyo inayompatia maisha, yeye na familia yake. Na kazi siyo ya kuajiriwa tu, hata ya kujiajiri kama ilivyo kwa wasanii.
Na unaposhindwa kufanya kazi, maana yake ni kwamba utashindwa kujimudu katika maisha kwa sababu kila kitu kinataka pesa.
Matokeo yake utaanza kuuza hata kidogo ulichonacho ili upate kuvuta. Utakapomaliza kuuza, bila shaka utawageukia marafiki na kuanza kuwaomba.
Obviously, watakuchoka!
Mimi ninawajua wasanii wanaovuta unga, wewe unawajua na hata wao wenyewe wanajijua. Kama ni ndugu yako, rafiki au jirani na unashindwa kumwambia, mwonyeshe kipande hiki akisome. Au ni wewe rafiki yangu msanii, achana na unga, mjanja wa kweli hali sembe bwana!

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: