April 14, 2014

UBINGWA WANUKIA LIVERPOOL, YAILAZA MAN CITY 3-2, COUTINHO BALAA LA MJINI!!

NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard  `Mr. Liverpool` ameangua kilio cha furaha baada ya timu yake kuukaribia thumbnail 1 summary

article-2603602-1D146FA400000578-379_634x539
NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard  `Mr. Liverpool` ameangua kilio cha furaha baada ya timu yake kuukaribia
ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.
Majogoo wa jiji kwa mara ya kwanza mwari anaanza kunukia kwao baada ya miaka 24 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya washindani wao wakubwa katika kinyang`anyiro cha  taji, Manchester City  Uwanja wa Anfield.
Bao lililoibua furaha nzito kwa Liverpool lilifungwa na Philippe Coutinho dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho.
Mabao mengine ya timu hiyo yalifungwa kipindi cha kwanza na Raheem Sterling dakika ya 6 na Martin Skrtel dakika ya 26.
Lakini City walikomaa na kusawazisha hadi kuwa 2-2 kwa mabao ya kipindi cha pili  ya David Silva katika dakika ya 75 na Glen Johnson aliyejifunga dakika ya 63.
Makosa ya Nahodha wa City, Vincent Kompany yalimpa Coutinho nafasi ya kufunga bao la  ushindi.
Baada ya mechi, Nahodha wa Wekundu hao wa Anifield, `Mr. Liverpool` Steven Gerrard alionekana kumwaga machozi kabla ya kuwakumbatia wachezaji wenzake.
Liverpool sasa inatimiza pointi 77 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kubarizi kileleni, wakati City inabaki na pointi zake 70 za mechi 32 na kuendelea kubaki nafasi ya tatu. Chelsea yenye pointi 75 za mechi 34 ni ya pili.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW: