Sean Combs, au unaweza kumuita P. Diddy na moja kati ya wasanii matajiri zaidi duniani, kwasasa jina lake la kisanii ni Puff Daddy.
japokua kwa maneno yake Combs, siku zote alikua ni Puff Daddy.
rapper/producer huyu ambaye anautajiri unaokadiriwa zaidi ya $700 million, alikua akijiita P. Diddy or Diddy kwa miaka 13 iliyopita, alidhibitisha kurejea kwa jina hilo kupitia account yake ya Twitter siku ya jumanne.
kubadilika kwa jina hilo kuna kuja sambamba na video ya Big Homie, ambayo inamsifia Puff Daddy (na sio Diddy) inapoanza. Track hiyo ipo kwenye album yake mpya ya MMM, inayotarajiwa kutoka mwaka huu.
Combs, ambae kipindi cha nyumba alikua akitoka na Jennifer Lopez, alijiita kwa maraya kwanza Puff Daddy mwaka 1997. Alibadilisha jina lake kuwa P. Diddy mwaka 2001, na kulifupisha kuwa Diddy mwaka 2005.