February 12, 2014

YOUND DEE AWA MBOGO KWA ANAYE TUMIA JINA LAKE KUTAPELI WATU MTANDAONI

Kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa watu maarufu kutokana na kuwepo kwa watu wanaofungua akaunti za facebook  kwa majina yao na kufa... thumbnail 1 summary


Kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa watu maarufu kutokana na kuwepo kwa watu wanaofungua akaunti za facebook  kwa majina yao na kufanya utapeli.

Rapper anaewakilisha kundi la Mtu Chee, Young Dee, amedai kuwa ingawa hayuko kabisa facebook, kuna mtu ambaye amekuwa akitumia jina lake kufanya utapeli licha ya kuzungumzia mara kwa mara kuhusu mtu huyo kwenye vyombo vya habari.

Rapper huyo wa ‘Kijukuu’, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa japokuwa alitangaza zawadi kwa mtu atakayefanikisha zoezi la kumpata mtu huyo bado hajafanikisha na kwamba mtu huyo anaendelea hadi leo.

Amesema aliwahi kwenda polisi kufungua mashitata dhidi ya mtu huyo akiwa na utambulisho wa BASATA kuwa yeye ndiye ‘Young Dee’, lakini polisi walidai ampeleke mtu ambaye ametapeliwa ndipo aweze kufungua kesi hiyo.

Tayari Young Dee ameshajipanga kwa ajili ya kuupeleka ushahidi utakaofanikisha zoezi la kumpandisha kizimbani tapeli anayetumia jina lake kwenye Facebook.

“Bado naendelea na zoezi langu, lakini sasa hivi nachokitafuta…kuna mtu wa sheria amenishauri kuna jinsi ambavyo hiyo kesi tunaweza kuifungua ikamake sense. Kwa hiyo ndio niko nae naconfirm naye, lakini bado tunakusanya ushahidi, kuna mtu mmoja nimempata ambaye ameshatapeliwa, natafuta mwiningine. Kwa hiyo tukishapata ushahidi wa kutosha tunaweza kum-sue. Young Dee ameiambia tovuti ya Times Fm.

Kama uko facebook na unachat na Young Dee, sanuka, jamaa hayuko facebook kabisa!

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments