January 24, 2014

UKWELI JUU YA KESI YA BENZEMA NA RIBERY, KUFANYA MAPENZI NA BINTI

Wachezaji soka wawili mashuhuri duniani wa timu ya taifa ya Ufaransa wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya n... thumbnail 1 summary
Wachezaji soka wawili mashuhuri duniani wa timu ya taifa ya Ufaransa wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono na kahaba aliyekuwa na umri mdogo Zahia Dehar . Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi alisema Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich alimtumia kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.
Inaripotiwa Ribery alimkatia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani mpaka Ufaransa kumtumbuiza wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo binti huyu anasema pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema wa Real Madrid. 
Benzema amekanusha madai ya msichana huyu kwamba aliwahi kulipwa pia kufanya nae ngono hotelini huko Paris wakati binti akiwa na umri wa miaka 16. Ribery amekubali kwamba kweli alifanya ngono na msichana huyu kama zawadi yake ya birthday lakini anasisitiza kwamba hakujua binti huyu hakuwa amefikisha umri wa miaka 18. Hawa wakali wa soka wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.

SHARE THIS POST TO SOCIAL MEDIA BELOW:

No comments