Raia mmoja wa kigeni amejikuta katika mtaro wa maji machafu
yaliyochanganywa kinyesi baada ya kipata ajali ya pikipiki maarufu kama
boda boda iliyogongwa na gari ambalo lilitoweka mara baada ya tukio
huku akikosa msaada kufuatia harufu mbaya aliyokuwa nayo.
Raia huyo ambaye hakuweza kupata msaada wa huduma
ya kwanza kwa wasamalia wema kama ilivyo ada ya Watanzania kabla ya
kutangaza donge nono kwa atakayemuosha kumwondolea tope hilo
lililochanganyika na kinyesi ili aweze kuelekea kupata huduma ya tiba.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo pamoja kulaumu
kukimbia kwa dereva aliwagonga walieleza tabia hiyo kuchagizwa na tabia
ya waendesha pikipiki kuwa wamekuwa chanzo cha madereva kutoweka mara
baada ya kuwagonga kutokana na tabia yao ya kujichukulia sheria mkononi
bara wanapopata ajali kwa inayhusisha magari na wengine kutumia fulsa
hiyo kuiba vitu kwenye magari.
No comments
Post a Comment