Baada
ya kimya kirefu juu ya tetesi za kurudiana kwa mwanadada Wema Sepetu na
Diamond kuzagaa kwenye mitandao hasa baada ya picha za wawili hao
waliokuwa wamechana kuonekana wakila “bata” pamoja maeneo ya Hong Kong
huko kwenye bara la Asia, sababu na ukweli wa namna wawili hao
walivyorudiana umewekwa waza baada ya hivi karibuni msanii diamond
platnumz kuzungumza na mtandao wa paparazi na kuelezea jinsi tukio hilo
zima lilivyokuwa.Katika
mazungumzo hayo Diamond alitaja mambo haya makuu matano yaliyosababisha
mpaka aamue kurudisha vikosi kwa mwanadada Sepetu.
Sababu ya kwanza (1) – UKARIMU WA WEMA
Diamond
alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema
kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.
“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna
vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema.
Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.
Akaongeza:
“Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume
aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.
“Kiukweli
nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule
mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.” Alisisitiza Diamond.
Sababu ya Pili (2) – Pamoja na Ukarimu – Mapokezi ya nguvu aliyopewa
Diamond
alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya
nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘Za Hatari’ na
kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.
Sababu ya tatu (3) – Ujasiri wa wema kwenda Hong Kong na kujiandaa kuwa mwenyeji wake.
Alifunguka
kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni
hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’
Sababu ya nne (4) – Mapenzi mazito aliyopewa huko Uchinani na Wema
Diamond
alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa
kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo
penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye.
Sababu ya tano (5) - Bado alikuwa na mawazo ya kupata mtoto na Wema
Diamond
alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye
anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo
katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.
Penny Je, hatima yake nini?
Hata hivyo, jitihada za kumtafuta
Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini
juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar
waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.
No comments
Post a Comment